Psalms 147

Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote


1 aMsifuni Bwana.

Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,
jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!


2 b Bwana hujenga Yerusalemu,
huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

3 cAnawaponya waliovunjika mioyo
na kuvifunga vidonda vyao.


4 dHuzihesabu nyota
na huipa kila moja jina lake.

5 eBwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,
ufahamu wake hauna kikomo.

6 f Bwana huwahifadhi wanyenyekevu
lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.


7 gMwimbieni Bwana kwa shukrani,
mpigieni Mungu wetu kinubi.

8 hYeye huzifunika anga kwa mawingu,
huinyeshea ardhi mvua,
na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.

9 iHuwapa chakula mifugo
na pia makinda ya kunguru yanapolia.


10 jFuraha yake haipo katika nguvu za farasi,
wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

11 k Bwana hupendezwa na wale wamchao,
wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.


12 lMtukuze Bwana, ee Yerusalemu,
msifu Mungu wako, ee Sayuni,

13 mkwa maana huimarisha makomeo ya malango yako
na huwabariki watu wako walio ndani yako.

14 nHuwapa amani mipakani mwenu
na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.


15 oHutuma amri yake duniani,
neno lake hukimbia kasi.

16 pAnatandaza theluji kama sufu
na kutawanya umande kama majivu.

17 qHuvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.
Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

18 rHutuma neno lake na kuviyeyusha,
huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.


19 sAmemfunulia Yakobo neno lake,
sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

20 tHajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote,
hawazijui sheria zake.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhKC